Indirimbo Zikundwa Open in the app

#154

E’ rafiki, shaka zako zipeleke kwake Yesu

Wokovu

Couplet 1

E’ rafiki, shaka zako zipeleke kwako Yesu! Aliyemwamini yeye hataona haya kamwe.

Refrain

Naamini, naamini, ninakuamini, Yesu. Naamini, naamini, naamini Neno lako.

Couplet 2

Dhambi zote ziungame na kwa Damu utakaswe, akuvike haki yake! Atakufikisha kwake.

Refrain

Naamini, naamini, ninakuamini, Yesu. Naamini, naamini, naamini Neno lako.

Couplet 3

Masumbuko yako yote uyaweke mbele yake! Ukipita uvulini, Bwana Yesu yupo nawe.

Refrain

Naamini, naamini, ninakuamini, Yesu. Naamini, naamini, naamini Neno lako.

Couplet 4

Na furaha yako pia ijulike kwake Yesu, Yeye, Bwana ju’ ya yote, akubarikie yote!

Refrain

Naamini, naamini, ninakuamini, Yesu. Naamini, naamini, naamini Neno lako.

Couplet 5

Ujitoe kwake Yesu: Roho, mwili na akili! Vyote vya maisha yako, anataka ku’takasa.

Refrain

Naamini, naamini, ninakuamini, Yesu. Naamini, naamini, naamini Neno lako.