#153
Yesu Kristo alifufuka akatoka
Wokovu
Couplet 1
Yesu Kristo alifufuka, akatoka kaburini. Furahini na msifuni, kwani alishinda kufa!
Refrain
Habari njema: Alifufuka katika wafu! Yesu yu hai, naye atakuja tena.
Couplet 2
Nguvu za mauti na dhambi Yesu Kristo alishinda; nasi sote tutashinda kwa nguvu yake ya ajabu.
Refrain
Habari njema: Alifufuka katika wafu! Yesu yu hai, naye atakuja tena.
Couplet 3
Kundi dogo, msiogope, Bwana Yesu ni uzima! Aliziondoa dhambi na anawafariji moyo.
Refrain
Habari njema: Alifufuka katika wafu! Yesu yu hai, naye atakuja tena.
Couplet 4
E’ Wakristo, shangilieni, Yesu aliyefufuka yu karibu, atakuja na atatufufua sote!
Refrain
Habari njema: Alifufuka katika wafu! Yesu yu hai, naye atakuja tena.