#139
Nina furaha kubwa, napumzika
Wokovu
Couplet 1
Nina furaha kubwa, napumzika sana, kwa kuwa nimefika kwa Mungu, Baba yangu. Ameniweka huru na mbali na utumwa, na sasa nakaa salama.
Couplet 2
Zamani nilidhani kuacha dhambi zote, lakini sikuweza kushinda peke yangu. Ninamwamini sasa Mwokozi wangu, Yesu, na yeye ananishindia.
Couplet 3
Mwokozi wangu, Yesu, aliyenifilia, aliokoa mimi, angali anipenda; nahesabiwa haki katika Damu yake, inayosafisha kabisa.
Couplet 4
Na nikijaribiwa na mwili wangu tena, ninakumbuka Yesu, apita vitu vyote. Neema yake kubwa kuliko dhambi zangu. Ninamshukuru Mwokozi.
Couplet 5
Na sasa Bwana Yesu akaa ndani yangu, Neema yake kubwa yanizunguuka mimi. Sitasumbuka tena, nimejiweka kwake, na Mungu anilinda vema.
Couplet 6
Shetani akitaka kufanya vita sasa, sitaogopa yeye na mamlaka yake. Maneno yake Mungu, ni yenye nguvu sana kwa wote wanaoamini.
Couplet 7
Ninaenenda sasa kwa jina lake Yesu, salama nitafika nyumbani mwa Babangu. Lakini safarini naimba siku zote, nikimshukuru Mwokozi.