Indirimbo Zikundwa Open in the app

#138

Sasa tayari kwetu siku ya kuokoka

Wokovu

Couplet 1

Sasa tayari kwetu siku ya kuokoka, Yesu alitimiza yote Msalabani. Wengi wanamjia Yesu Mwokozi wao, wapate kustarehe, wapone nafsi zao.

Refrain

Mwana-kondo’ wa Mungu tunakusifu sana! Uzima uliweka kwa’jili yetu sisi. Umetufanya kuwa mitume yake Mungu. Kati’ majina yote lako ni kubwa mno.

Couplet 2

Wewe kwa Damu yako ulikomboa sisi, na jua la Neema linatuangazia. Tumefahamu sasa pendo la Mungu wetu. Damu imetuunga kati’ agano jipya.

Refrain

Mwana-kondo’ wa Mungu tunakusifu sana! Uzima uliweka kwa’jili yetu sisi. Umetufanya kuwa mitume yake Mungu. Kati’ majina yote lako ni kubwa mno.

Couplet 3

Njoo upesi nawe uliyesitasita! Mungu atakujaza Neema yake kubwa, raha rohoni mwako inayokutuliza, matumaini, nguvu, pendo lililo bora.

Refrain

Mwana-kondo’ wa Mungu tunakusifu sana! Uzima uliweka kwa’jili yetu sisi. Umetufanya kuwa mitume yake Mungu. Kati’ majina yote lako ni kubwa mno.