Indirimbo Zikundwa Open in the app

#121

Yesu ni furaha yangu

Wokovu

Couplet 1

Yesu ni Furaha yangu, amejaa Pendo kweli. Anaweza kusimika kila mwenye udhaifu. Ananipa ujasiri, nguvu, raha na faraja. Hata nikionja kufa, Yesu ni mchunga wangu.

Couplet 2

Nimefungwa na Mwokozi kwa kifungu cha upendo, hata kufa hakuwezi kunitenga naye Yesu. Mimi wake siku zote, ninataka kumtii. Kwa Neema nimepona, nisitumikie dhambi.

Couplet 3

Kwa mikono ya upendo ninakumbatiwa naye, sitaweza kutafsiri pendo lake kubwa kwangu. Napokea nguvu yake, yanijaza moyo wangu. Yesu ananiongoza katika safari yangu.