#104
Lo! Horini Bethlehemu
Wokovu
Couplet 1
Lo! Horini Bethlehemu, ndani ’nyumba ya ng’ombe, Bwana Yesu alilala usingizi wa kitoto. Nyota zilizo Mbinguni kimya ziliangazia Bwana Yesu, mtulivu, juu ya ulalo wake.
Couplet 2
Wachungaji wa kondoo walikuja kumwabudu, na majusi walifika wakamtolea tunu. Mungu mwenye macho yanayo tazama nchi yote, alivunja makusudi ya kuua ya adui.
Couplet 3
Nakupenda, Bwana Yesu, kwani unaufaamu udhaifu wa mtoto, hali yake ya kitoto. Nawe sasa unaweza kunisaidia sana kila saa ya hatari, majaribu na mashaka.
Couplet 4
Nakuomba, Bwana Yesu, unilinde njia yote, uwe mwenzi wangu Mwema kila saa na dakika! Usichoke nami kamwe, nami sitaona hofu; Yesu unikumbatie siku zote na milele!