#102
Sayuni, ulaki Bwanako
Wokovu
Couplet 1
Sayuni, ulaki Bwanako, umshangilie Mfalme! Jipambe kwa Bwana arusi, ujitengeneze tayari!
Refrain
Furahi, furahi! Umshangilie Bwanako! Furahi, furahi! Umsujudie Mfalme!
Couplet 2
Kutoka ’tukufu wa Baba na kiti cha enzi Mbinguni Mwokozi alitufikia kulazwa mtoto horini.
Refrain
Furahi, furahi! Umshangilie Bwanako! Furahi, furahi! Umsujudie Mfalme!
Couplet 3
Akawa dhabihu kamili, akasulibiwa Golgotha, akafa kwa ’ajili ya wote, tupewe Wokovu wa Mungu.
Refrain
Furahi, furahi! Umshangilie Bwanako! Furahi, furahi! Umsujudie Mfalme!
Couplet 4
Alitushindia mauti na kumharibu shetani; akaufunua uzima, tupate kuishi milele.
Refrain
Furahi, furahi! Umshangilie Bwanako! Furahi, furahi! Umsujudie Mfalme!
Couplet 5
Afika kwa wenye huzuni kuwapa faraja na heri, na atamiliki milele, Mfalme wa pendo na haki.