Indirimbo Zikundwa Open in the app

#101

E’ mlinzi, twauliza

Wokovu

Couplet 1

E’ mlinzi, twauliza: Yesu atakuja lini? Asubuhi ya Sayuni ni karibu? Tuambie! Msafiri, yainue macho yako, angalia! Asubuhi ni karibu, usimame, usimame!

Couplet 2

Siku heri ya Sabato ya milele ni karibu, na dalili yake Yesu hapo itaonekana. Na rohoni tunaona nchi nzuri ya ahadi. Asubuhi ni karibu, na Ahadi zatimia.

Couplet 3

Katika Yerusalemu, Mji mpya wa Mbinguni, Yesu atatumiliki kwa Upendo na amani. Baragumu italia, nasi tutaisikia. Yesu ni karibu sana kutukaribisha kwake.