#93
Siku chache, na tena Wakristo
Wokovu
Couplet 1
Siku chache, na tena Wakristo watakwenda kumwona Mwokozi, siku chache na wataipewa thawabu na taji ya uzima.
Refrain
Nangoja sana Bwana Yesu kama zamu angojavyo asubuhi. :/: Kwa dalili zote ninaona sasa kwamba Yesu yu karibu ya kurudi:/:
Couplet 2
Siku chache za vita ya huku, tena Yesu Mfalme atakuja; tutaona furaha na raha, atatupeleka kwake juu.
Refrain
Nangoja sana Bwana Yesu kama zamu angojavyo asubuhi. :/: Kwa dalili zote ninaona sasa kwamba Yesu yu karibu ya kurudi:/:
Couplet 3
Siku chache machozi ya shida, Mungu atayafuta kabisa. Na baada ya siku si nyingi kwa lango nitaingia Mbingu.
Refrain
Nangoja sana Bwana Yesu kama zamu angojavyo asubuhi. :/: Kwa dalili zote ninaona sasa kwamba Yesu yu karibu ya kurudi:/:
Couplet 4
Baragumu la mwisho ’talia, waminifu watachukuliwa; wote wataingia Mbinguni kukaa pamoja na Mwokozi.