Indirimbo Zikundwa Open in the app

#92

Yesu! Jina hili linapita kila jina

Wokovu

Couplet 1

Yesu! Jina hili linapita kila jina duniani pote. Yesu, Yesu! Jina hilo ni marhamu iliyomiminwa.

Refrain

Jina hili ni lenye nguvu ya kuondoa dhambi zangu zote. Yesu, Yesu! Jina hilo lanitia shangwe na furaha.

Couplet 2

Si jingine jina duniani lenye nguvu, kweli na uzima. Yesu, Yesu! Jina hilo waliloimbia malaika.

Refrain

Jina hili ni lenye nguvu ya kuondoa dhambi zangu zote. Yesu, Yesu! Jina hilo lanitia shangwe na furaha.

Couplet 3

Jina hili lina wema mno, limejaza Mbingu tangu mwanzo. Yesu, Yesu! Jina hilo, litaimbwa duniani pote.

Refrain

Jina hili ni lenye nguvu ya kuondoa dhambi zangu zote. Yesu, Yesu! Jina hilo lanitia shangwe na furaha.

Couplet 4

Sitaweza kusahahu Yesu, jina lake ni Wokovu wangu. Yesu, Yesu! Nitamwona huko kwake tena kwa furaha.