#64
Kimya e’ moyo wangu
Wokovu
Couplet 1
Kimya, e’moyo wangu, mbele za Bwana Yesu! Unahitaji sana ’kaa daima kwake. Njia salama ipi ulimwenguni huku bila kumfuata Yesu na neno lake?
Refrain
Uniongoze, Bwana, katika njia yako! Hata ikiwa shida nitawasili kwako.
Couplet 2
Kimya, e’moyo wangu, omba kwa tumaini! Nuru itatokea ukiamini Mungu, na umwambie Yesu shaka uliyo nayo, atakuosha sana, atakuonya njia.
Refrain
Uniongoze, Bwana, katika njia yako! Hata ikiwa shida nitawasili kwako.
Couplet 3
Kimya, e’moyo wangu, msikilize Mungu! akuletea nguvu, tena hekima kweli. Na ukiendelea katika neno lake, Mungu atakujaza nguvu na uthabiti.
Refrain
Uniongoze, Bwana, katika njia yako! Hata ikiwa shida nitawasili kwako.