#63
Yesu, nivute karibu nawe
Wokovu
Couplet 1
Yesu, nivute karibu nawe, ’kiwa kwa shida, ikiwa kwa raha! Uliyekufa Msalabani, :/: ’nifaamishe upendo na ne’ma! :/:
Couplet 2
Yesu, nivute, mimi maskini, sina vipaji vya kukutolea, moyo ninao wenye udhaifu, :/: Uupokee, ’uoshe kwa Damu! :/:
Couplet 3
Yesu, nivute, nikutolee yote ninayo, e’ Bwana mpendwa, ninakuomba: Uyaondoe :/: yote yanayo nitenga na Mungu! :/:
Couplet 4
Yesu, nivute karibu nawe hata ukomo wa vita na shida! Tena Mbinguni nitakuwapo :/: karibu nawe, e’ Yesu Mwokozi! :/: