Indirimbo Zikundwa Open in the app

#11

Ikiwa wananiuliza

Wokovu

Couplet 1

Ikiwa wananiuliza msingi wa uzima, Je, twahitaji kuongeza kwa kazi yake Yesu? Kwa uhodari nitajibu: Msingi wangu ni wa nguvu, ni Damu yake Yesu Kristo, inanitosha sana.

Couplet 2

U Mwamba wa zamani sana, daima utadumu. Na hata siku nitakufa, nitautegemea. Nitakapoondoka huku, nitamsifu mwana kondoo, na Damu ya Mwokozi wangu, funguo la Mbinguni.