#203
Safari yangu sasa
Umuco
Couplet 1
Safari yangu sasa, iko wazi kweli; kwakuwa nimejua mimi ni nani, na nimejua kuwa msafiri ni nini, na shaba ya msafiri ni nini.
Refrain
Njia nimeijua, na mwisho wake nimeujua, na wasafiri ninawajua, waliyo wa kwetu nawajua, Haleluya nasifu Bwana, Haleluya, haleluya!
Couplet 2
Nimeona mengi, humu safarini, nimejua wengi humu safarini, na hali za wasafiri nimezijua, kitu gani kitanishimamisha tena.
Refrain
Njia nimeijua, na mwisho wake nimeujua, na wasafiri ninawajua, waliyo wa kwetu nawajua, Haleluya nasifu Bwana, Haleluya, haleluya!
Couplet 3
Tabia za kwetu ninazijua, zisizo za kwetu ninazijua; wamaneno mengi nimewajua, Haleluya, haleluya, nimewajua!
Refrain
Njia nimeijua, na mwisho wake nimeujua, na wasafiri ninawajua, waliyo wa kwetu nawajua, Haleluya nasifu Bwana, Haleluya, haleluya!
Couplet 4
Mitego yote nimeijua, habari za uongo zote nimezijua habari za Ufalme piya nimezijua, ni nani atakae nidanganya tena?
Refrain
Njia nimeijua, na mwisho wake nimeujua, na wasafiri ninawajua, waliyo wa kwetu nawajua, Haleluya nasifu Bwana, Haleluya, haleluya!
Couplet 5
Ninafurahi sana humu safarini, kwakuwa sitapotea njia tena kwa nguvu ya Mungu yote nimeyijua, ni nakwenda mbinguni, Haleluya.