#581
Mwokozi wangu ni uzima
Umuco 2
Couplet 1
Mwokozi wangu ni uzima, Unaodhihirika, Ameingia rohoni mwangu, Sasa anafurika; {Njoni nyote Ndugu tuchangie, Chakula cha Uzima.} x2
Couplet 2
Sote tunazaa matunda mengi, Tumepata Uzima, Naomba Bwana Atuongezeye, Uzima wake tele; {Tupate kuwa na Ushindi wote, Tukanyage Adui zetu.} x2
Couplet 3
Nilipoteza muda wangu, katika usingizi, Nilikuwa jeshi asiyejua Sauti ya Kiongozi; {Nimegundua siri ya Uzima, Kushika Neno lote.} x2
Couplet 4
Katika siku za Safari, Bwana ameniongoza, Nilitenda Maovu ya utoto, Bwana akavumilia; {Upendo wake wapita fahamu, Ni Mzazi Mwema kweli.} x2
Couplet 5
Kwa hatua yangu ya sasa, Bwana nifunguwe Macho, Ili nione vema kwa uwazi, uzito wa Kazi yako; {Bwana zibua sikio za Roho, Nijue Mapito yako.} x2
Couplet 6
Nilipoteza muda wangu, Pasipo Wokovu, Lakini kwa huruma wako Mungu Umeniangazia; {Umenipa Imani halisi, Na Matumaini hai.} x2
Couplet 7
Bwana wangu Yesu nashukuru, Uzima ulionipa, Jicho Lako lisitoke kwangu, usiku na mchana; {Niwapende Ndugu zangu hawa, Vitani pa Uzima.} x2