#428
Natembea nachunguza
Umuco 2
Couplet 1
Natembea nachunguza duniani, Njia yangu nipitayo ni ndefu sana, Shida nyingi na majaribu vyanizunguka Simba wamo wananguruma... wanangununa.
Refrain
Nitamtazama Bwana Yesu, Yeye ni Mshindaji wa Njia hii, Vita vikija mbele yangu, Yesu ni Mshindaji Atavishinda, {Ameutowa uhai wake, Ajili yetu sisi kondoo.} x2
Couplet 2
Bwana Yesu ni Mshindaji wetu Mwema A’tangulia sisi kondoo kwenda mbele, A’tuita sisi sote tumfuate, Aduwi wote wa Bwana Yesu Atawashinda.
Refrain
Nitamtazama Bwana Yesu, Yeye ni Mshindaji wa Njia hii, Vita vikija mbele yangu, Yesu ni Mshindaji Atavishinda, {Ameutowa uhai wake, Ajili yetu sisi kondoo.} x2
Couplet 3
Nashukuru Mungu Baba wa Upendo Kumtuma Mwana wake kutufilia, Bwana Yesu ‘kashimamisha Bendera nzuri Ya Damu yake ambayo kwa hiyo, twaokolewa.
Refrain
Nitamtazama Bwana Yesu, Yeye ni Mshindaji wa Njia hii, Vita vikija mbele yangu, Yesu ni Mshindaji Atavishinda, {Ameutowa uhai wake, Ajili yetu sisi kondoo.} x2
Couplet 4
Bwana Yesu akaitoa Damu yake, Ajili yetu, ili tupate Wokovu wake, kwa Upendo wa Mungu Baba tutashinda Aduwi wote, Bwana Yesu Atawashinda.