#158
Mimi ni msafiri katika duniya
Umuco
Couplet 1
Mimi ni msafiri katika dunia ninasafiri, katika safari ninaishi katika vita vya ajabu, ninapigana na vita vya kila aina, mimi ni msafiri na askari vitani.
Refrain
Jameni Ni nawezaje Mimi, kuwa musafili kamili, nisipo juwa hali za msafiri? Jameni ninawezaje mimi, kuwa askari kamili, nisipopigana vita? mimi ni msafiri na askari vitani.
Couplet 2
Mimi ni msafiri, katika dunia, ninakutana na jaribu njiani. Nina kutana na masimba njiani, ninapigana na kila jaribu, mimi ni msafiri na askari vitani.
Refrain
Jameni Ni nawezaje Mimi, kuwa musafili kamili, nisipo juwa hali za msafiri? Jameni ninawezaje mimi, kuwa askari kamili, nisipopigana vita? mimi ni msafiri na askari vitani.
Couplet 3
Mimi ni msafiri, katika dunia na nina ushindi katika safari, njiani simba ninazishinda, milima ninaipanda sana, nina mshindaji karibu nami.
Refrain
Jameni Ni nawezaje Mimi, kuwa musafili kamili, nisipo juwa hali za msafiri? Jameni ninawezaje mimi, kuwa askari kamili, nisipopigana vita? mimi ni msafiri na askari vitani.
Couplet 4
Mimi ni msafiri, katika dunia, jaribu linanipa kuwa macho, linanipa kuamka na kujijua, jaribu linanipa kujiadhari sana, jalibu linanipa kuwa na ufahamu.
Refrain
Jameni Ni nawezaje Mimi, kuwa musafili kamili, nisipo juwa hali za msafiri? Jameni ninawezaje mimi, kuwa askari kamili, nisipopigana vita? mimi ni msafiri na askari vitani.
Couplet 5
Mara ninapokutana na jaribu, ndipo ninaamka uzimani mwangu, kama sijaribiwe ninajisahau, lakini sasa silali vitani mimi, ninapigana vita vizuri sana.