#134
Haleluya kwa bwana Yesu
Umuco
Couplet 1
Haleluya, Haleluya! Kwa Bwana Yesu Kristo kwa sababu Kazi ya Mungu, (Inaendelea sana) katika upepo, (Inaendelea sana) katika moto, (Inaendelea sana) katika vyote, (Inaendelea sana.)
Refrain
Ingawa ukichoka, ingawa nikichoka, ingawa wakipinga Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, ina Pembe la nguvu Haleluya, Haleluya, Haleluya!
Couplet 2
Haleluya, Haleluya! Kwa Bwana Yesu Kristo, kwa sababu Guzo ya moto inasonga mbele sana, Wana wa Mungu wanaifuata sana, Wateule wa Mungu wanaifuata sana, katika vyote, wanaendelea sana.
Refrain
Ingawa ukichoka, ingawa nikichoka, ingawa wakipinga Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, ina Pembe la nguvu Haleluya, Haleluya, Haleluya!
Couplet 3
Haleluya, Haleluya! Kwa Bwana Yesu Kristo Yeye ndie Msingi wa kazi ameweka Msingi Gologotha Kazi ya Mungu inaendelea sana, waliyo wake, wanaiona uwazi, wasio wake wanafia janguani walio wake, watafika Sayuni.
Refrain
Ingawa ukichoka, ingawa nikichoka, ingawa wakipinga Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, ina Pembe la nguvu Haleluya, Haleluya, Haleluya!
Couplet 4
Haleluya, Haleluya! Kwa Bwana Yesu Kristo Yeye ndie Jiwe la Uzima, jiwe wajengaji waliyo gaili, limegeuka Jiwe lishikalo pembe, limegeuka, jiwe la Msingi wa nguvu, limegeuka Jiwe lishikalo Nyumba.
Refrain
Ingawa ukichoka, ingawa nikichoka, ingawa wakipinga Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, ina Pembe la nguvu Haleluya, Haleluya, Haleluya!
Couplet 5
Ebu ndugu yangu sasa, lisiwe Jiwe la kukwaza, kwako na kwangu pia ndugu, katika hatua zake Mungu liwe Jiwe la Uzima kwangu mimi, liwe jiwe la Uzima na kwako ndugu, ili tupate kuishi milele na milele.