Indirimbo Zikundwa Open in the app

#112

Enyi wana wa Mungu

Umuco

Couplet 1

Enyi wana wa Mungu sikiyeni habari njema, habari ya kufariji habari ya ufalme, si habari ingine kunyakuliwa kwa Kanisa kwakaribia.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza kulikua kwa Enoki, kunyakuliwa kwa pili kulikuwa kwa Elia, kunyakuliwa kwa tatu ni kwa Kanisa, kwakalibia.

Couplet 2

Enoki alikua Mgeni asiye kuwa na hila, alikua akimpenda Mungu, maishani mwake, alikua akitembea pamoja na Mungu, kisha akanyakuliwa.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza kulikua kwa Enoki, kunyakuliwa kwa pili kulikuwa kwa Elia, kunyakuliwa kwa tatu ni kwa Kanisa, kwakalibia.

Couplet 3

Na Elia alimpenda Mungu kupita vyote, alikubali kuteswa juu yake alimtumikia Mungu kushinda wote, akatembea naye, kisha akanyakuliwa.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza kulikua kwa Enoki, kunyakuliwa kwa pili kulikuwa kwa Elia, kunyakuliwa kwa tatu ni kwa Kanisa, kwakalibia.

Couplet 4

Bwana Yesu alikuja duniani humu, kutafuta Bibi Arusi wake, aliacha ahadi, kwa Bibi Arusi, kwamba atakuja kumchukua ajitayalishe.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza kulikua kwa Enoki, kunyakuliwa kwa pili kulikuwa kwa Elia, kunyakuliwa kwa tatu ni kwa Kanisa, kwakalibia.

Couplet 5

Bibi Arusi anangoja ahadi ya Bwana Arusi, Hata wengine wamchekeleye, yeye ni umoja na ahadi na huyo Bibi Arusi ni mwili wa Kristo, Haleluya.