Indirimbo Zikundwa Open in the app

#103

Wanao tabiri ni wengi

Umuco

Couplet 1

Wanao tabiri ni wengi, wanao jazwa ni wengi sana; wapakwa mafuta ni wengi; wafanya ishara ni wengi ./.Kilicho vema kwangu ni kuongozwa na neno la Mungu./.

Couplet 2

Waponya magonjwa ni wengi, na wa kuita ni wengi; wahubiri nao ni wengi, na waalimu ni wengi ./.Kilicho vema kwetu ni kujaa neno la Mungu./.

Couplet 3

Wasema Bwana, Bwana ni wengi, na watumishi ni wengi; wanao onya ni wengi, wanao jitowa ni wengi ./.Kinacho nifurahisha mimi ni kufuata nyayo za Bwana./.

Couplet 4

Duniani wa nabii ni wengi, na wajuaji ni wengi, wenye maarifa ni wengi; watenda mema ni wengi ./.Lakini mimi ni mtoto wa nyumbani mwa Baba Mungu./.

Couplet 5

Kilicho muhimu sana, kati ya mambo yote, ni kujaa neno la Mungu, na kuongozwa nalo ./.Na kujua mapenzi ya neno ndicho kilicho vema kati yote./.