#298
Bwana amesema
Umuco 1
Refrain
[Trad. en Kir., voir Cant. n°464]
Couplet 1
Bwana amesema tumpingeni, Huyo Shetani na yeye pia, Atatukimbia, ni ahadi, Tuliyopewa na Bwana Yesu.
Refrain
{Kweli tutashinda... tutashinda, Tukiamini Neno, Tutashinda kwa nguvu za Bwana, Tukafike mbinguni.} x2
Couplet 2
Pia Bwana amesema tumu-, karibiye Yeye peke, Na Yeye atatukaribia, Huo ndiyo ushindi wetu.
Refrain
{Kweli ni ushindi... ni ushindi, Kweli ushindi ni wetu, Tukidumu katika imani, Tutashinda kwa nguvu za Bwana.
Couplet 3
Kumbukeni Abrahamu pale, Mlimani Moriya amejari, -biwa sana na kwa imani, Ameshinda majaribu yote.
Refrain
{Basi tutashinda... tutashinda, Tukishikamana na Neno, Na kubaki katika imani, Tutamuona Bwana Yesu.} x2