Indirimbo Zikundwa Open in the app

#185

Mara nyingi ninateswa

Umuco 1

Couplet 1

Mara nyingi ninateswa, Na ubaya wa dunia, Maovu yanisumbua, Ninyakue nije kwako, Nikae Yerusalemu.

Refrain

E’ Mbingu jiandae, E’ Yerusnlemu jiandae, Jiandaeni kupokea, Walioshinda dunia, Wanaokuwa na kovu, Za Msalaba wa Kristo.

Couplet 2

Ahadi zote zimefika, Dalili zote zimefika, Umemtuma Eliya, Kuandaa Kanisa lako, Tunyakue tuje kwako.

Refrain

E’ Mbingu jiandae, E’ Yerusnlemu jiandae, Jiandaeni kupokea, Walioshinda dunia, Wanaokuwa na kovu, Za Msalaba wa Kristo.

Couplet 3

Tarumbeta ya malaika, Wa siku za mwisho imelia, Tunangojea nini Baba? Tufariji na Roho wako, Tukungojee kwa bidii.

Refrain

E’ Mbingu jiandae, E’ Yerusnlemu jiandae, Jiandaeni kupokea, Walioshinda dunia, Wanaokuwa na kovu, Za Msalaba wa Kristo.

Couplet 4

Umenyakua Enoki, Umenyakua Eliya, Walikuwa wamechukizwa, Na maasi ya dunia, Tunyakue nasi Bwana.

Refrain

E’ Mbingu jiandae, E’ Yerusnlemu jiandae, Jiandaeni kupokea, Walioshinda dunia, Wanaokuwa na kovu, Za Msalaba wa Kristo.

Couplet 5

Ashindae atavikwa, Taji ya uzima wa milele, Ataishi Yerusalemu, Pamoja na Mkombozi, Milele na milele.