Indirimbo Zikundwa Open in the app

#134

(retouché)

Umuco 1

Couplet 1

Haleluya, haleluya, Kwa Bwana Yesu Kristo! Kwa sababu kazi ya Mungu, {Inaendelea sana.} x2 - Katika (u)pepo, {Inaendelea sana.} x2 - Katika moto, {Inaendelea sana.} x2 - Katika vyote, {Inaendelea sana.} x2

Refrain

Ingawa ukichoka, Ingawa nikichoka, Ingawa wakipinga, Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, Ina pembe la nguvu, Haleluya, Haleluya, Haleluya.

Couplet 2

Haleluya, haleluya, Kwa Bwana Yesu Kristo! Kwa sababu nguzo ya moto, Inasonga mbele sana, Wana wa Mungu, * Wanaifuata sana, - Wateule wake, * Wanaifuata sana, - Katika yote, * Wanaendelea sana.

Refrain

Ingawa ukichoka, Ingawa nikichoka, Ingawa wakipinga, Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, Ina pembe la nguvu, Haleluya, Haleluya, Haleluya.

Couplet 3

Haleluya, haleluya, Kwa Bwana Yesu Kristo! Yeye ndiye msingi wa kazi, (A)meweka msingi Goligotha, - Kazi ya Mungu, * Inaendelea sana, - Walio wake, Wanaiona uwazi, - Wasio wake, * Waangamia jangwani.

Refrain

Ingawa ukichoka, Ingawa nikichoka, Ingawa wakipinga, Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, Ina pembe la nguvu, Haleluya, Haleluya, Haleluya.

Couplet 4

Haleluya, haleluya, Kwa Bwana Yesu Kristo! Yeye ni Jiwe likwazalo, Ndiye Jiwe la uzima, - Limegeuka, * Jiwe lishikalo pembe, - Limegeuka, * Jiwe la msingi wa nguvu, - Limegeuka, * Jiwe lishikalo nyumba.

Refrain

Ingawa ukichoka, Ingawa nikichoka, Ingawa wakipinga, Kazi ya Mungu inaendelea, Ina Msingi mkubwa, Ina Mwamba mkubwa, Ina pembe la nguvu, Haleluya, Haleluya, Haleluya.

Couplet 5

Ebu ndugu yangu sasa, Lisiwe jiwe la kukwaza, Kwako na kwangu pia ndugu, Kati hatua zake Mungu, - Na liwe Jiwe, * La uzima kwangu mimi, - Na liwe Jiwe, * La uzima kwako ndugu, - Ili tupate, * Kurithi ufalme milele.