#114
Ulitoka huko misri
Umuco 1
Couplet 1
Ulitoka huko Misri, bondeni mwa uovu., Ukavuka bahari nyekundu, ukakuwa wa Yesu, Mungu akakuvukisha bahari nyekundu, Ukaanza safari ya kwenda Sayuni, Uwe tayari katika safari.
Refrain
Jiepushe na kiburi, Jiepushe na mwili, Jiepushe na akili, Jiepushe na uvivu, Jiepushe na ujuaji, Ambatana na hekima, Utakua mwenye heri siku zote.
Couplet 2
Uliona nguzo ya moto, uliona manu kushuka, Mwamba nao ukapasuka, Na wafalme wakashindwa, Uliona mambo mengi katika jangwa, Iyo haitoshi, ambatana na Yosua, Usije ukafia jangwani.
Refrain
Jiepushe na kiburi, Jiepushe na mwili, Jiepushe na akili, Jiepushe na uvivu, Jiepushe na ujuaji, Ambatana na hekima, Utakua mwenye heri siku zote.
Couplet 3
Uliona nguvu za Mungu katika vyote uwazi, Unajua njia za Mungu na mapito yake yote, Lakini iyo haitoshi, zidisha kumuona, Wengi katika Israeli wameona yote, Lakini wameishia jangwani.
Refrain
Jiepushe na kiburi, Jiepushe na mwili, Jiepushe na akili, Jiepushe na uvivu, Jiepushe na ujuaji, Ambatana na hekima, Utakua mwenye heri siku zote.
Couplet 4
Waweza kuwa katika taifia hilo la ajabu, Lakini wewe kama haukuwi kama Kalebu, Na wewe utaishia jangwani ndugu, Usichokee ndani ya wokovu, Jiepushe ujuaji wako.