Indirimbo Zikundwa Open in the app

#112

Enyi wana wa Mungu

Umuco 1

Couplet 1

Enyi wana wa Mungu, Sikieni habari njema, Habari ya kufariji, habari ya ufalme, Si habari ingine: kunyakuliwa, kwa Kanisa kwakaribia.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza: Kulikuwa kwa Enoki, Kunyakuliwa kwa pili: Kulikuwa kwa Elya, Kunyakuliwa kwa tatu: Ni kwa Kanisa... kwakaribia.

Couplet 2

Enoki alikuwa mgeni, Asiyekuwa na hila, Alikuwa akimpenda Mungu, maishani mwake, Alikua akitembea pamoja na, Mungu kisha akanyakuliwa.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza: Kulikuwa kwa Enoki, Kunyakuliwa kwa pili: Kulikuwa kwa Elya, Kunyakuliwa kwa tatu: Ni kwa Kanisa... kwakaribia.

Couplet 3

Na Eliya alimpenda Mungu kupita, vyote, Alikubali kuteswa juu yake, Alimtumikia Mungu kushinda wote, Akatembea naye kisha akanyakuliwa.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza: Kulikuwa kwa Enoki, Kunyakuliwa kwa pili: Kulikuwa kwa Elya, Kunyakuliwa kwa tatu: Ni kwa Kanisa... kwakaribia.

Couplet 4

Bwana Yesu alikuja duniani humu, kutafuta Bibi-arusi wake, Aliacha ahadi kwa Bibi-arusi, Kwamba atakuja kumchukua, ajitayarishe.

Refrain

Kunyakuliwa kwa kwanza: Kulikuwa kwa Enoki, Kunyakuliwa kwa pili: Kulikuwa kwa Elya, Kunyakuliwa kwa tatu: Ni kwa Kanisa... kwakaribia.

Couplet 5

Bibi-arusi anangoja ahadi, ya Bwana-arusi, Hata wengine wamchekeleye, Yeye ni umoja na ahadi, Na huyo Bibi-arusi, Ni mwili wa Kristo, Haleluya!