#106
Chini ya mbingu mimi
Umuco 1
Couplet 1
Chini ya mbingu mimi, Nimechunguza kilicho chema, Ili nipate kukichagua, Lakini nimeona yote ni ya bure, Heri kwenda mbinguni.
Refrain
Vilivyo dunia ni bure, Dunia ni bonde la mauti, Kilicho chema kwangu mimi, Ni kutoka katika dunia hii, Niende mbinguni kwa Baba.
Couplet 2
Niliona mimi, Kuchagua ufalme na mambo, Yalio makuu juu ya yote, Lakini nimeona yote ni ya bure, Yote ni bonde la mauti.
Refrain
Vilivyo dunia ni bure, Dunia ni bonde la mauti, Kilicho chema kwangu mimi, Ni kutoka katika dunia hii, Niende mbinguni kwa Baba.
Couplet 3
Nimeona kilicho juu, Ya mambo yote huku chini, Ni kuchagua kama Yakobo, Ni kuchagua kurithiwa Ufalme, Na kupandishwa mbinguni.
Refrain
Vilivyo dunia ni bure, Dunia ni bonde la mauti, Kilicho chema kwangu mimi, Ni kutoka katika dunia hii, Niende mbinguni kwa Baba.
Couplet 4
Niliulizwa jambo, Huku chini va mbingu: “Nitachagua nini katika yote?”, Nilichagua kurithi Ufalme, Na kupandishwa mbinguni.
Refrain
Vilivyo dunia ni bure, Dunia ni bonde la mauti, Kilicho chema kwangu mimi, Ni kutoka katika dunia hii, Niende mbinguni kwa Baba.
Couplet 5
Marafiki wananichukia, Eti nimechagua vibaya, Waniona kama mpumbavu, Lakini nimeona kilicho juu ya yote, Ni kuchagua uzima.