Indirimbo Zikundwa Open in the app

#96

Mbingu za mbingu zimefunguliwa

Umuco

Couplet 1

Mbingu za mbingu zimefunguliwa kwa ajili yako mwaminifu; uliempokea Bwana Yesu, milango yote iko wazi kwa wale waliomwamini karibia uingie Uzimani.

Refrain

./.Njoo Mwaminifu uingie katika lango hilo lango limefunguliwa Bwana Yesu Amelifungua./.

Couplet 2

Milango yote imefungwa kwa wale wasiomwamini, wanangojea kuteketezwa, kila kazi ya mtu itapimwa, waruka ukuta watapimwa matendo yote yatapimwa.

Refrain

./.Njoo Mwaminifu uingie katika lango hilo lango limefunguliwa Bwana Yesu Amelifungua./.

Couplet 3

Mtu mwenye kujipendekeza na mambo ya kukufuru, uyo si mwana wa Ufalme watoto wa Kora na Balamu wajaana kiburi, majivuno hawapite katika lango.

Refrain

./.Njoo Mwaminifu uingie katika lango hilo lango limefunguliwa Bwana Yesu Amelifungua./.

Couplet 4

Mlango sasa uko wazi kwa wale wanao uona, wanao jua Mwokozi wao, vizuri vyajaana umwo vilivyo andaliwa wote wanaopita mlangoni.

Refrain

./.Njoo Mwaminifu uingie katika lango hilo lango limefunguliwa Bwana Yesu Amelifungua./.