Indirimbo Zikundwa Open in the app

#79

Tafuteni ufalme wake bwana.

Umuco

Couplet 1

Tafuteni Ufalme wake Bwana, na Nguvu za Ufalme tafuteni Uzima wake Bwana; ./.Vingine vitatufuata./.

Refrain

Ufalmeni mwa Baba kunajaa Upendo Ufalmeni mwa Baba kunajaa Amani Ufalmeni mwa Baba kunajaa Furaha ./.Ni sifa kwa Bwana wetu./.

Couplet 2

Tafuteni vizuri vya Ufalme na Utajiri usio oza; tafuteni vazi la Arusi ./.Ishara zitatufuata./.

Refrain

Ufalmeni mwa Baba kunajaa Upendo Ufalmeni mwa Baba kunajaa Amani Ufalmeni mwa Baba kunajaa Furaha ./.Ni sifa kwa Bwana wetu./.

Couplet 3

Tafuteni Uso wake Bwana na Utukufu wake, tafuteni Upendo wake Bwana ./.Karama zitatufuata./.

Refrain

Ufalmeni mwa Baba kunajaa Upendo Ufalmeni mwa Baba kunajaa Amani Ufalmeni mwa Baba kunajaa Furaha ./.Ni sifa kwa Bwana wetu./.

Couplet 4

Tuzifuate Nyayo zake Bwana na Bidii Alikua nayo; tuenende kama Alivyo enenda ./.Tutarithi Ufalme./.

Refrain

Ufalmeni mwa Baba kunajaa Upendo Ufalmeni mwa Baba kunajaa Amani Ufalmeni mwa Baba kunajaa Furaha ./.Ni sifa kwa Bwana wetu./.

Couplet 5

Tukiwa na uzima wake Bwana; karama zitatumika tukiwa na nguvu zake Bwana ./.Vyote tutavipata./.