Indirimbo Zikundwa Open in the app

#139

Nuru ya rohoni

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu. Nakuomba sana niangazishe; ukanitazame kwa huruma tu,

Refrain

Ukanitulize mimi maskini.

Couplet 2

Futa dhambi zangu kwa damu yako. Hasira ya Mungu iniondoke. Machubuko yako, hata mateso,

Refrain

Niyawaze vema rohoni mwangu.

Couplet 3

Nakutumaini peke yako tu, niwe mtumwa wako pote nilipo utanikubali sina mashaka!

Refrain

Nitakushukuru pasipo mwisho.