Indirimbo Zikundwa Open in the app

#129

Karibu na Wewe

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Karibu na Wewe, Mungu wangu Karibu zaidi, Bwana wangu Siku zote niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.

Couplet 2

Mimi nasafiri Duniani, Pa kupumzika Sipaoni, Nilalapo niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.

Couplet 3

Na kwa nguvu zangu Nikusifu; Mwamba, uwe maji Ya Wokovu; Mashakani niwe Karibu na wewe; Karibu zaidi Mungu wangu.

Couplet 4

Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Zikikoma hapa Siku zangu, Kwa furaha niwe Pamoja na wewe, Karibu kabisa Mungu wangu.