Indirimbo Zikundwa Open in the app

#107

Ewe Baba wa Mbinguni

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombalo Hapa chini duniani, Na uwe radhi nalo

Refrain

Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!

Couplet 2

Watu hawa mbele zako, Na mbele ya kanisa; Watimize Neno lako Wanakutana sasa.

Refrain

Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!

Couplet 3

Kama Yesu na Kanisa, Ni mmoja, na hivyo, Watu hawawape sasa Wawe mmoja vivyo

Refrain

Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!

Couplet 4

Walinde, Bwana, daima, Wabariki nyumbani Uwape nyingi salama Humu ulimwenguni.

Refrain

Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!

Couplet 5

Wabariki, ewe Bwana, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli.

Refrain

Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!

Couplet 6

Siku za duniani Zitakapopungua, Wape kurithi Mbinguni Mema ya kwendelea.