Indirimbo Zikundwa Open in the app

#63

Ndugu wa kirohoni

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ndugu wa kirohoni Mliokombolewa, Tafakarini sana Yatupasayo.

Refrain

Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.

Couplet 2

Siku itatimia Tutakapoulizwa Wale wa nyumba zetu Na majirani

Refrain

Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.

Couplet 3

Tujitoeni, ndugu, Tukahubiri Injili. Atutumie Roho kuponya wengi.

Refrain

Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.

Couplet 4

Wasiokombolewa Ni wengi vijijini, Wataokolewaje Tukiogopa?

Refrain

Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.

Couplet 5

Bwana alijitoa Akapotewa mengi, Ili atuokoe, Tusiwe waoga.

Refrain

Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.

Couplet 6

Aliyetununua, Kwa kuimwaga damu, Angalieni sana Msimwepuke.