Indirimbo Zikundwa Open in the app

#62

Bwana wa mabwana

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Bwana wa mabwana, Mwenye nguvu sana Twakusihi: Neno la milele Na liende mbele, Waongoke tele Kwa Mwokozi.

Couplet 2

Tunawaona Wanavyopatana, Kulipinga, Hawataliweza Neno, kulitweza: Huwaje! Kucheza: Na upanga?

Couplet 3

Heri wajitunze Ili wapatane, Na Mwokozi; Watafute sana, Wapate kuona, Yesu kuwa Bwana, Mkombozi.

Couplet 4

Mungu awaita Wasije kukuta Pigo lake; Hakuona vyema Wakose uzima, Awape rehema, Waokoke.

Couplet 5

Mwenye utukufu Tunamshukuru Yeye pweke! Nasifiwe sana, Baba, naye Mwana, Na wa tatu tena Roho yake.