#296
Yesu Anataka tungae
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Yesu Anataka tungae kwetu Kama taa ya kuwa usiku; Giza linazidi duniani huko; Wewe ngaa kwako na mimi kwangu.
Couplet 2
Yesu anataka tungae safi, Tusiache kitu kupunguza nuru; Anarutazama toka kule Mbingu, Wewe ngaa kwako na mimi kwangu.
Couplet 3
Yesu anataka tungae kwake Watu wengi wasikie Neno lake; Na watoke giza kuingia nuru, Wewe ngaa kwako na mimi kwangu.