#251
Bwana, fungua macho yangu
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Bwana, fungua macho yangu Kwa kufahamu Neno lako; Unionyeshe mambo matamu Ndani ya Neno lako, Bwana.
Refrain
Ninainama sasa kwako, unionyeshe kweli yako, Vile mapenzi yako, Bwana, ninakusihi.
Couplet 2
Bwana, fungua masikio kwa Neno lako nisikie, Kwani sauti yako ni tamu, inanichunga kwa jaribu.
Refrain
Ninainama sasa kwako, unionyeshe kweli yako, Vile mapenzi yako, Bwana, ninakusihi.
Couplet 3
Bwana, fungua kinywa changu Niwe tayari kutangaza Kwa wapotevu kila pahali, wewe uliwakufilia.
Refrain
Ninainama sasa kwako, unionyeshe kweli yako, Vile mapenzi yako, Bwana, ninakusihi.