Indirimbo Zikundwa Open in the app

#188

Yesu Mwokozi Alinikufia

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Yesu Mwokozi Alinikufia, Naye amenipa uzima mupya; Nikitazama Mwokozi daima, Kila dakika naishi kwa Bwana.

Refrain

Kila dakika nachungwa na Yesu, Kila dakika napata uzima; Nikitazama Mwokozi daima, Kila dakika naishi kwa Bwana.

Couplet 2

Kwa majaribu, mateso na taabu, Yesu Mwokozi ananishindisha, Na anabeba mizigo ya roho; Kila dakika ananisaidia.

Refrain

Kila dakika nachungwa na Yesu, Kila dakika napata uzima; Nikitazama Mwokozi daima, Kila dakika naishi kwa Bwana.

Couplet 3

Saa ya huzuni, machozi, uchungu, Saa ya hatari, saa ya uzaifu, Hata Mwokozi ni kule Mbinguni, Kila dakika ananifikili.

Refrain

Kila dakika nachungwa na Yesu, Kila dakika napata uzima; Nikitazama Mwokozi daima, Kila dakika naishi kwa Bwana.

Couplet 4

Hata ugonjwa unanikamata, Yesu anaweza kuniponyesha; Hata katika maneno yo yote, Kila dakika ananichungaga.