Indirimbo Zikundwa Open in the app

#187

Kama una mahitaji

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Kama una mahitaji, huna mali nyingi tena, Njaa vile ikifika kwako nyingi, Ukumbuke Mungu Baba analinda kila saa, Leta taabu yako yote kwake Yesu.

Refrain

Uiache yote kwake, Acha taabu yako yote kwake Yesu; Ukimusadiki Mungu, atakupatisha nguvu, Acha taabu yako yote kwake.

Couplet 2

Wewe ni mugonjwa vile, mwili unauma sana, Taabu inaleta woga mwingi kwako? Yesu anajua yote naye atakusaidia, Leta taabu yako yote kwake Yesu.

Refrain

Uiache yote kwake, Acha taabu yako yote kwake Yesu; Ukimusadiki Mungu, atakupatisha nguvu, Acha taabu yako yote kwake.

Couplet 3

Kama wewe ni muzee, unachoka sikuzote, Ee, usisahau Mungu yuko nawe; Yesu ni karibu sasa, na atakuchunga sana, Leta taabu yako yote kwake Yesu.

Refrain

Uiache yote kwake, Acha taabu yako yote kwake Yesu; Ukimusadiki Mungu, atakupatisha nguvu, Acha taabu yako yote kwake.