#141
Usimame kwa ahadi zake Kristo
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Usimame kwa ahadi zake Kristo, Sasa na milele umusifu sana; Leta utukufu wote kwake Mungu, Usimame kwa ahadi zake.
Refrain
Usimame, leo usimame kwa ahadi zake; Usimame, simama kwa ahadi zake Mungu.
Couplet 2
Usimame kwa ahadi za milele, Hata majaribu yanatesa sana; Utapata nguvu kwa Maneno yake, Usimame kwa ahadi zake.
Refrain
Usimame, leo usimame kwa ahadi zake; Usimame, simama kwa ahadi zake Mungu.
Couplet 3
Usimame kwa ahadi zake Bwana, Kwani unafungwa kwa milele kwake, Roho atakushindisha sikuzote, Usimame kwa ahadi zake.
Refrain
Usimame, leo usimame kwa ahadi zake; Usimame, simama kwa ahadi zake Mungu.
Couplet 4
Usimame kwa ahadi, hutaanguka, Ukisikiza Roho akiita: Upumzike ndani ya Mwokozi wako, Usimame kwa ahadi zake.
Refrain
Usimame, leo usimame kwa ahadi zake; Usimame, simama kwa ahadi zake Mungu.