Indirimbo Zikundwa Open in the app

#126

Na hali yangu ninakuja

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Na hali yangu ninakuja pasipo neno ila moja: Ulimimia Damu yako, ninakuja kwako, Bwana.

Couplet 2

Na hali yangu sitangoja kujisafisha kosa moja; Kwa damu utaniokoa, ninakuja kwako, Bwana.

Couplet 3

Na hali yangu kwa matata, mashaka, woga na azabu, Nipate raha kwako, Mungu, ninakuja kwako, Bwana.

Couplet 4

Na hali yangu masikini, kipofu, bule, na zaifu, Nipate mali ya milele, ninakuja kwako, Bwana.

Couplet 5

Na hali yangu ninaamini ahadi zako zote kweli; Nipate usamehe wako, ninakuja kwako, Bwana.