#117
Mimi mwenye makosa nilikombolewa
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Mimi mwenye makosa nilikombolewa, Mwokozi alipojitoa; Zambi zangu na zako alizichukua, Kwa damu aliniokoa.
Refrain
Zambi zangu zilimutundika Mwokozi Alipojitoa Kalvari; Alizarauliwa na kukataliwa Atupatanishe na Mungu.
Couplet 2
Yesu mwenye upole na mwenye mapendo Ananitakasa rohoni; Nimepata uhuru kwa Yesu Mwokozi, Alikufa Musalabani.
Refrain
Zambi zangu zilimutundika Mwokozi Alipojitoa Kalvari; Alizarauliwa na kukataliwa Atupatanishe na Mungu.
Couplet 3
Namwambata Mwokozi, sitaki kumwacha, Kwa kuwa alinikufia; Nakusifu, Ee Yesu, unayenipenda, Daima nakushangilia.
Refrain
Zambi zangu zilimutundika Mwokozi Alipojitoa Kalvari; Alizarauliwa na kukataliwa Atupatanishe na Mungu.