#112
Unakubali kuacha makosa?
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Unakubali kuacha makosa? Kwa Damu ya Yesu kuna uwezo; Na unataka kushinda Shetani Kwa Damu ya Yesu Mwokozi?
Refrain
{Kuna nguvu ya ajabu kubwa, Ndiyo Damu ya Mwokozi.} x2
Couplet 2
Unakubali kuvunja tamaa? Kwa Damu ya Yesu kuna uwezo; Kuja upate usafi wa moyo Kwa Damu ya Yesu Mwokozi?
Refrain
{Kuna nguvu ya ajabu kubwa, Ndiyo Damu ya Mwokozi.} x2
Couplet 3
Unakubali kuoshwa moyoni? Kwa Damu ya Yesu kuna uwezo; Vitaondoshwa vipaku vya zambi Kwa Damu ya Yesu Mwokozi?
Refrain
{Kuna nguvu ya ajabu kubwa, Ndiyo Damu ya Mwokozi.} x2
Couplet 4
Unakubali kutenda vizuri? Kwa Damu ya Yesu kuna uwezo; Na unataka kufika Mbinguni Kwa Damu ya Yesu Mwokozi?
Refrain
{Kuna nguvu ya ajabu kubwa, Ndiyo Damu ya Mwokozi.} x2