Indirimbo Zikundwa Open in the app

#98

Nimekombolewa kabisa

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Nimekombolewa kabisa, nitaitangaza daima; Nimekombolewa na Yesu, na mimi ni wake milele.

Refrain

Nimekombolewa na Damu ya Yesu Mwokozi; Nimekombolewa, na mimi ni wake milele.

Couplet 2

Kwa Yesu furaha ni nyingi, kuliko furaha nyingine; Najua yeye ni karibu na tunabakia pamoja.

Refrain

Nimekombolewa na Damu ya Yesu Mwokozi; Nimekombolewa, na mimi ni wake milele.

Couplet 3

Ninamufikili saa zote, Mwokozi muzuri wa watu; Mapendo makubwa ni yake, Kwa hivi naimba na nguvu.

Refrain

Nimekombolewa na Damu ya Yesu Mwokozi; Nimekombolewa, na mimi ni wake milele.

Couplet 4

Najua nitamutazama Mufalme Mupenzi Mbinguni, Anayenichunga na pendo, kunipa furaha moyoni.

Refrain

Nimekombolewa na Damu ya Yesu Mwokozi; Nimekombolewa, na mimi ni wake milele.