#83
Nilizama kwa makosa
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Nilizama kwa makosa, katika maji ya zambi; Roho yangu iliona kufa na giza tele; Mungu alinisikia nilipomulilia, Akanipandisha na kuniokoa.
Refrain
{Nimeokoka, nimeokoka, Kwa Yesu Mukombozi nimeokoka.} x2
Couplet 2
Sasa Yesu amekuwa Makimbilio yangu; Pendo lake kubwa sana liko moyoni mwangu; Neema yake ya kuzidi inanijaza roho; Niwe mwaminifu kwake siku zote.
Refrain
{Nimeokoka, nimeokoka, Kwa Yesu Mukombozi nimeokoka.} x2
Couplet 3
Nawe mwenye sikitiko, kuna matumaini; Yesu anakufahamu na atakusaidia; Atakupandisha toka tope la kuteleza; Upokee Neema yake kwa Wokovu.
Refrain
{Nimeokoka, nimeokoka, Kwa Yesu Mukombozi nimeokoka.} x2