Indirimbo Zikundwa Open in the app

#82

Yesu kwa muji wa Betelehemu

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Yesu kwa muji wa Betelehemu Alizaliwa katika taabu; Ninashangaa sababu Mwokozi alitafuta mimi. Alitafuta mimi, alitafuta mimi, Ninashangaa sababu Mwokozi alitafuta mimi.

Couplet 2

Yesu Mwokozi, zamani Kalvari Deni ya zambi alinilipia; Kuniletea uhuru wa kweli alinikufilia. Alinikufilia, alinikufilia, Kuniletea uhuru wa kweli alinikufilia.

Couplet 3

Yesu Mwokozi alinikumbuka Nami ningali tu mbali na Baba, Na siku zote alinitafuta, akiniita mimi. Akiniita mimi, akiniita mimi, Na siku zote alinitafuta, akiniita mimi.

Couplet 4

Yesu Mwokozi aliniahidi Atarudia kutoka Mbinguni, Na nitamwona katika mawingu, atanitwaa kwake. Atanitwaa kwake, atanitwaa kwake, Na nitamwona katika mawingu, atanitwaa kwake.