Indirimbo Zikundwa Open in the app

#74

Ni Neema ya kunishangaza

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Ni Neema ya kunishangaza iliyoniokoa; Nilipotea, lakini Yesu alinivuta kwake.

Couplet 2

Hukumu ya Mwamuzi Mungu niliogopa sana; Lakini sasa, kwa Neema yake, sitaogopa tena.

Couplet 3

Katika majaribu mengi nimesimama nguvu; Kwa Neema yake alinichunga, hataniacha kamwe.

Couplet 4

Tutashukuru Mungu wetu milele na milele Kwa Neema kubwa tuliyoona katika Mwana wake.