Indirimbo Zikundwa Open in the app

#246

Kale nilitembea gizani

Izindi

Couplet 1

Kale nilitembea gizani, dhambi zikanifunga mno. Alipiga hodi Yesu Kristo, mlangoni pa roho yangu.

Refrain

Alikuja Yesu gizani mwa roho yangu, nilimkaribisha Aingie, Giza Akaliondoa.

Couplet 2

Akaingia Yesu Mwokozi, Akanifurahisha sana. Kweli hakuna Mungu mwingine, kuwaokoa wakosaji.

Refrain

Alikuja Yesu gizani mwa roho yangu, nilimkaribisha Aingie, Giza Akaliondoa.

Couplet 3

Akafanya vita msalabani, Akashinda adui wote. Akanipa uwezo rohoni, Akashinda mamlaka yote.

Refrain

Alikuja Yesu gizani mwa roho yangu, nilimkaribisha Aingie, Giza Akaliondoa.

Couplet 4

Atanilinda hata milele, Upendoni mwake Mwokozi. Nitamtumikia duniani, vilevile Mbinguni kwake.

Refrain

Alikuja Yesu gizani mwa roho yangu, nilimkaribisha Aingie, Giza Akaliondoa.