#176
Ndani ya chicha
Iz'i Gisenyi
Couplet 1
Ndani ya chicha la tai kuna miiba chini na juu kuna majani na pamba, wana wa tai hulala juu ya pamba majani mpaka mabawa takavyo ota:x2
Refrain
Ndipo sasa mama tai naye akitafuta kufundisha wanae kujua kuruka.x2 Ataondoa ndani chicha majani na pamba yote watoto hulaliya miiba.x2 Miiba iwatobowapo watatafuta kuepuka wakiyapiga mabawa yao.x2 Mabawa itatiwa nguvu kwa mazowezi hayo mpaka wataanza kuruka Hewani.x2 Mazowezi haya ya Tai hakuna hata na kunguru moja yaweza kuyavumiliya.x2
Refrain
S: Siku B: Siku moja S: Moja B: Siku moja S: mama B: mama tai S: Tai B: mama tai S: tawa B: Tawatupa S: Tupa B: Tawatupa Hewani wapate kuruka. S: waka B: Wakati S: Tiwa B: Wakati S: Shindwa B: washindwa S: Kuruka B: Washindwa S: mama B: mama tai S: Tai B: mama tai huwabeba kwa mabawa yake.x2
Couplet 2
Baba yetuu ni tai nasi tuwana tai twalishwa mudomo kwa mudomo. Ameetupa maisha ya mazowezi pamoja nayeye.x2
Refrain
Kitafuta kutufundisha ngisi yakupigana vita taacha adui kutuvuruga.x2 Kitafuta kutufundisha ngisi yakupigana vita taacha shida zituupate.x2 Zoruba nyingi kanisani magonjwa, njaa, mafundisho mageni yote hutushambuliya.x2 Mambo haya tuyaonapo niyakawayida chichani na yote ni ya mafaa yetu. x2 Kama wewe si mwana tai utakapoona vipimo utakimbiya kanisa lako.x2
Refrain
S: Waka B: Wakati S: Pitwa B: Wakati S: Shindwa B: twashindwa S: vipimo B: twashindwa S: mama B: mama tai S: tai B: mama tai huja upesi kutusaidiya.x2