#145
Nafanya mwendo
Iz'i Gisenyi
Couplet 1
Nafanya mwendo siku kwa siku nasitacoka sijamaliza yote, natumaini kufika Mbingu kwa Inchi iliyo kwa mawingu. Nina furahi kwa ajili ya Wokovu tuliopata kutoka kwake Mungu, kati Safari yafaa shangwe kwani twaenda kwake Mwokozi.
Refrain
Nafanya vita ya kushinda adui Upanga wangu ni Neno lake Mungu na kwa maombi ninasimama natazamiya Ahadi zake. Nashika njia katika vita kali adui wanizunguka pande zote namutazama Mwokozi wangu nikiwa naye siogope kitu.
Couplet 2
Safari yangu maisha yangu nina ambiwa kuvumilia yote, natumaini kufika Mbingu kati Uwezo wa Mungu wangu. Nakombolewa katika Neema kubwa, na kwa Imani naendelea mbele, namufuata Mwokozi wangu Aliye kufa kwa ajili yangu.
Refrain
Nafanya vita ya kushinda adui Upanga wangu ni Neno lake Mungu na kwa maombi ninasimama natazamiya Ahadi zake. Nashika njia katika vita kali adui wanizunguka pande zote namutazama Mwokozi wangu nikiwa naye siogope kitu.
Couplet 3
Anaye acha ndugu na nyumba baba na mama watoto na mashamba kwa ajili ya Jina lake Yesu na juu Injili ya Mungu. Ni mara miya atapokeya huko kwa Mbingu tena Uzima wa milele, anaye mutumikiya Yesu Mungu atamuheshimu sana.
Refrain
Nafanya vita ya kushinda adui Upanga wangu ni Neno lake Mungu na kwa maombi ninasimama natazamiya Ahadi zake. Nashika njia katika vita kali adui wanizunguka pande zote namutazama Mwokozi wangu nikiwa naye siogope kitu.
Couplet 4
Shetani aja kwa njiya yangu kunionyesha uzuri wa dunia, huniambiya ni mufuate nitapokea heshima kwake. Sitafuata Shetani hata kufa uzuri wake ni wa muda kitambo, machozi yananitoka mengi kwa hiyo vita ya kila siku.