#492
Ee bwana ninakuhitaji
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Ee Bwana ninakuhitaji sana, Siku zote maishani mwangu; Pasipo Wewe sitaweza kitu, Nakusihi, Bwana, kaa nami.
Refrain
Kaa nami, ninakuhitaji, Kaa nami, majaribu yaja, Kaa nami, wakati wowote Siku zote, Bwana, kaa nami.
Couplet 2
Adui wanapo nishambulia, Upepo mawimbi yakivuma; Wakati ninapo-ogopa sana, Nakusihi, Bwana, kaa nami.
Refrain
Kaa nami, ninakuhitaji, Kaa nami, majaribu yaja, Kaa nami, wakati wowote Siku zote, Bwana, kaa nami.
Couplet 3
Na Katika safari yangu huku, Unilinde na kuniongoza, Na mateso yanaponizidia, Nakusihi, Bwana, kaa nami.
Refrain
Kaa nami, ninakuhitaji, Kaa nami, majaribu yaja, Kaa nami, wakati wowote Siku zote, Bwana, kaa nami.
Couplet 4
Hakuna awezaye kuokoa, Ila Wewe pekee Yako Bwana, Na Wewe pekee ndiwe Mkombozi, Nakusihi, Bwana, kaa nami.