#393
Unakuja, ee mwokozi
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Unakuja, ee Mwokozi, unakuja, Mfalme, Kila ulimi takiri Jina Lako, ee Bwana; Unakuja, tutaimba kwa furaha na shangwe. Safari yetu ‘takwisha, tutakaa na Wewe.
Refrain
Unakuja, unakuja tutakuona Bwana, Unakuja, unakuja Tutafanana Nawe; Unakuja, unakuja Yesu Bwana Mpendwa: Furaha gani kuona uso Wako, ee Bwana.
Couplet 2
Unakuja siku ile utafuta machozi, Zambi, shida na mateso hayo yote’ takwisha; Tutaiacha dunia na mambo yake yote, Tutayasahau yote itakuwa furaha.
Refrain
Unakuja, unakuja tutakuona Bwana, Unakuja, unakuja Tutafanana Nawe; Unakuja, unakuja Yesu Bwana Mpendwa: Furaha gani kuona uso Wako, ee Bwana.
Couplet 3
Unakuja mawinguni pamoja ‘malaika, Kwa sauti Yako kubwa wafu watafufuka, Na sisi tulio hai, o tutabadilika, Sote tutanyakuliwa kukutana na Wewe.
Refrain
Unakuja, unakuja tutakuona Bwana, Unakuja, unakuja Tutafanana Nawe; Unakuja, unakuja Yesu Bwana Mpendwa: Furaha gani kuona uso Wako, ee Bwana.
Couplet 4
Unakuja, twakungoja, tunajua ni kweli, Hatujui siku na saa, twajua u karibu; Unakuja, tutakula mezani Nawe Bwana Kwa Karamu ya Arusi Yake Mwana Kondoo.